Mapenzi ya 
Diamond na Penny sasa yameenda next level kwani sasa wanatarajia kuitwa mama na 
baba nanilihu miezi michache ijayo, yote hayo yamejulikana katika kipindi cha 
XXL ya Clouds Fm na Gossip Cop ambapo Diamond alisema ni kweli Penny ambaye ni 
mtangazaji wa DTV ni mjamzito na wanatarajia kupata mtoto, 
Soudy Brown 
alimuuliza kuhusu fununu za kutumia Milioni 15 kununua gari la mke wake 
mtarajiwa Penny 
Diamond 
amekiri kwamba ni kweli kamnunulia Penny gari kwa sababu anaelekea kuwa mama 
watoto ambapo namkariri akisema “nilimuuliza gari gani anapenda, nimemuagizia 
iko njiani inakuja siwezi kusema ni bei gan ila kwa sasa anatumia la muda wakati 
akisubiria gari lake”
Alipoulizwa 
kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond amejibu “siwezi 
kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza ikawa harusi ila kuna time 
inafika inabidi utulie, siwezi kusema chochote kwa sababu inawezekana mtoto 
akazaliwa ndani ya ndoa pia “

No comments:
Post a Comment