Yaani 
Wanawake kwa kupenda Pete dah,Mungu awasaidie. Mtu una ndoto zako maskini, kubwa 
tu, Mungu kakupa akili nzuri tu, ila anatokea mtu from nowhere, wala hata sio 
type yako, humpendi kiivyo, ila kisa kaja na Ring basi mnasisimka kama mmeguswa 
na Jini Subiani.
Akishakupa 
mpete wa bati akasema; 'Honey, ntakuoa', yaani mnakuwa kama mmepigwa nusu kaputi 
za Maternity Room, mnayeyuka kama Koni za Azam, unasahau kabisa kila ndoto 
uliyonayo, Unamkabidhi Tunutu alinde shamba la uwele!
Kuna girls 
wameolewa na watu wasio sahihi wameua ndoto zenu za kusoma, mlikuwa mnataka 
mjiendeleze Jamaa halitaki, linakuuliza unasoma ili iweje?? Unataka unizidi 
kipato, Myopic Brained-husband! Na wengine wakiona tu umejaza fomu za Chuo Kikuu 
wanakulia timing wanakutundika mimba, ukiwaza kuweweseka na Kitumbo cha ujauzito 
na kufanya assignment za class, mwenyewe una-surrender, una-forego Elimu kisa 
pete, ujuha huo!
Girls, 
msiue ndoto zenu kisa umeahidiwa Pete na juha moja lisilotambua Priorities zako, 
kama anakupenda ataku-support positively on ur plans, huyo ndo mume, kama 
umeplan kusoma, soma kwanza, pete zipo! Kama umeplan kujenga jenga kwanza 
usikimbilie ndoa utageuzwa Incubator kutotoa mfululizo na hata veranda 
hutamaliza... Pete ni mbati tu wa duara usiharibu akili zenu, Ur dreams come 
first, Pete si uchonge hata mwenyewe kwa sonara Mwenge?? WanaaumeTumeshajua 
mnapenda sana pete, tunawavisha, na tutawavisha sana hadi viunoni kama shanga, 
mnakuwa watumwa wetu kiulaini!
WAKE 
UP!!!
SOURCE: 
SETH DE JESUS GIOVANN
No comments:
Post a Comment